Luke 22:60 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Petro akasema, “Bwana wee; sijui hata unachosema!” Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Petro akasema, “Wewe, wala sijui unazungumza kuhusu nini!” Alipokuwa bado anazungumza, jogoo aliwika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Petro akasema, “Bwana wee; sijui hata unachosema!” Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Petro akasema, “Bwana wee; sijui hata unachosema!” Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati uo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Petro akasema, “Bwana wee; sijui hata unachosema!” Na papo hapo, akiwa bado anaongea, jogoo akawika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Petero akasema: Mwenzangu, sijui, unavyosema. Angali akisema, papo hapo jogoo akawika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Petro akasema: “Sijui mambo unayoyasema.” Wakati ule alipokuwa angali akisema, jogoo akawika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro akasema, Ewe mtu, sijui unenalo. Papo hapo alipokuwa akisema yeye, jogoo akawika.