Luke 22:61 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Bwana Isa akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Bwana aligeuka akamtazama Petro kwenye macho yake. Kisha Petro akakumbuka Bwana alivyokuwa amesema ya kwamba, “Kabla ya jogoo kuwika asubuhi, utakuwa umenikana mara tatu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Bwana akageuka akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka yale maneno ambayo Bwana alimwambia, “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Bwana Isa akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana Isa alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana akageuka na kumtazama Petro, naye Petro akakumbuka yale aliyokuwa ameambiwa na Bwana: “Leo kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipomgeukia Petero, amtazame; hapo Petero akalikumbuka lile neno la Bwana, kama alivyomwambia: Jogoo atakapokuwa hajawika leo, utakuwa umenikana mara tatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana akageuka na kumwangalia Petro. Petro akakumbuka maneno yale Bwana aliyomwambia kwamba mbele jogoo hajawika atakuwa amemukana mara tatu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bwana akageuka, akamtazamisha Petro: Petro akalikumbuka neno la Bwana, jinsi alivyomwambia, Kabla hajawika jogoo leo, utanikana marra tatu.