Luke 22:66 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulipopambazuka, Baraza la Wazee, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, wakakutana pamoja, naye Isa akaletwa mbele yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alfajiri, viongozi wazee wa watu, viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walikusanyika. Walimpeleka Yesu kwenye baraza lao kuu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na walimu wa Sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulipopambazuka baraza la wazee wa watu, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulipopambazuka, baraza la wazee wa watu, yaani viongozi wa makuhani na walimu wa Torati, wakakutana pamoja, naye Isa akaletwa mbele yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulipokucha, wakakusanyika wazee wa kwao na watambikaji wakuu na waandishi, wakampeleka barazani kwa wakuu wao wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Usiku ulipokucha, wazee wa Wayuda, wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria, wakakusanyika. Wakamuleta Yesu mbele ya Baraza yao Kubwa,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta ulipokuwa mchana wakakusanyika jamii ya wazee wa watu, na makuhani wakuu, na waandishi, wakamleta kwa haraza yao, wakisema,