Luke 23:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Herode pamoja na askari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Herode na askari wake wakamdhihaki Isa na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Herode na askari wake wakamcheka. Wakamfanyia mzaha kwa kumvalisha mavazi kama ambayo wafalme huvaa. Kisha Herode akamrudisha Yesu kwa Pilato.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, herode pamoja na maaskari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Herode pamoja na askari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Herode na maaskari wake wakamdhihaki Yesu na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Herode na askari wake wakamdhihaki Isa na kumfanyia mzaha. Wakamvika vazi zuri sana, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Herode akamdhalilisha, pamoja na askari wake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Herode pamoja na askari wake, wakamwaibisha Yesu na kumfanyia mzaha; kisha wakamvika vazi la kifalme, wakamrudisha kwa Pilato.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Herode pamoja na askari wake walipokwisha kumbeza na kumfyoza, akamvika nguo nyeupe imetukayo, akamrudisha kwa Pilato!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi Herode na waaskari wake wakamuchekelea Yesu na kumuzarau. Wakamuvalisha nguo zinazokuwa sawa za mufalme na kumurudisha kwa Pilato.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi Herode akamtweza pamoja na askari zake akamdhihaki, akamvika mavazi mazurimazuri, akamrudisha kwa Pilato.