Luke 23:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pilato akawaambia mara ya tatu, “Amefanya ubaya gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mara ya tatu Pilato akawaambia watu, “Kwa nini? Amefanya kosa gani? Hana hatia. Sioni sababu ya kumwua. Hivyo nitamwachia huru baada ya kumwadhibu kidogo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Pilato akawaambia mara ya tatu, “Amefanya kosa gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pilato akawaambia mara ya tatu, “Amefanya ubaya gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa mara ya tatu Pilato akawaambia, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yo yote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi na kisha nitamwachia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa mara ya tatu, Pilato akawauliza, “Kwani amefanya kosa gani huyu mtu? Sikuona kwake sababu yoyote inayostahili adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe mijeledi, na kisha nitamwachia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pilato akawaambia mara ya tatu, “Amefanya ubaya gani? Sioni kosa lolote kwake linalomstahili auawe; kwa hiyo nitampiga viboko, halafu nimwachilie.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowauliza mara ya tatu: Ni kiovu gani, alichokifanya huyu? Sikuona neno kwake la kumhukumu, auawe; basi, nitampiga, kisha nitamfungua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pilato akawaambia kwa mara ya tatu: “Alifanya ubaya gani? Mimi sikumwona na hata kosa moja linalomustahili kuhukumiwa kufa. Nitaamuru apigwe fimbo, na kisha nitamufungua.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akawaambia marra ya tatu, Kwani? ubaya gani alioutenda huyu? sikuona hatta neno kwake la kustahili kufa; bassi nikiisha kumrudi nitamfungua.