Luke 23:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa kusababisha uasi na mauaji; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Isa mikononi mwao, wamfanyie watakavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walitaka Baraba aliyekuwa gerezani kwa sababu ya kuanzisha fujo na mauaji aachiwe huru. Pilato akamwachia Baraba. Na kumtoa Yesu ili auawe. Hili ndilo watu walitaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa sababu ya uasi na kuua; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa kusababisha uasi na mauaji; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfanyie watakavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamfungua yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika uasi dhidi ya serikali na mauaji. Akamkabidhi Isa mikononi mwao, wamfanyie watakavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akamfungua kutoka gerezani yule waliyemtaka, ambaye alikuwa ametiwa gerezani kwa kusababisha uasi na mauaji; akamtoa Yesu kwao, wamfanyie walivyotaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamfungua yule aliyetiwa kifungoni kwa ajili ya kondo na ya kuua watu, ndiye waliyemtaka; lakini Yesu akamtoa, wamfanyizie watakavyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamufungua yule mutu waliyetaka, aliyefungwa kwa ajili ya kuleta fujo na kuua watu, na kumutoa Yesu kwao kusudi wamutendee vile walivyotaka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamfungua yeye aliyetiwa gerezani kwa fitina na uuaji, waliyemtaka: akatoa Yesu kwa mapenzi yao.