Luke 23:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni Mkirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Askari wakamwongoza Yesu kumtoa nje ya mji. Wakati huo huo mtu mmoja kutoka Kirene alikuwa anaingia mjini kutoka maeneo nje ya Yerusalemu. Askari wakamlazimisha kuubeba msalaba wa Yesu na kumfuata Yesu kwa nyuma.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja, aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anatoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shambani, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipompeleka wakamshika Simoni wa Kirene aliyepita akitoka shambani, wakamtwika msalaba, amchukulie Yesu na kumfuata.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walipokuwa wakimupeleka Yesu kwenda kutundikwa, wakakutana na mutu mumoja aliyeitwa Simoni, wa inchi ya Kurene, aliyekuwa akitoka kwenye vijiji. Wakamulazimisha abebe musalaba wa Yesu na kumufuata nyuma.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.