Luke 23:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na Yesu alikuwa anasema, “Baba uwasamehe watu hawa, kwa sababu hawajui wanalofanya.” Askari waligawana nguo zake kwa kutumia kamari.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akasema: Baba, waondolee! Kwani hawajui wafanyayo.* Hata nguo zake wakazipigia kura, wazigawanyiane.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akasema: “Baba uwasamehe, kwa maana hawajui jambo wanalofanya.” Waaskari wakagawanya nguo zake kwa kuzipigia kura.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.