Luke 23:46 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Alipokwisha sema hayo, akakata roho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipaza sauti akasema, “Baba, ninaiweka roho yangu mikononi mwako!” Baada ya Yesu kusema haya, akafa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, naiweka roho yangu mikononi mwako.” Alipokwisha sema hayo, akakata roho.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Alipokwisha sema hayo, akakata roho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akalia kwa sauti kubwa: “Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.” Alipokwisha sema hayo, akakata roho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akapaza sauti kuu akisema: Baba, roho yangu naiweka mikononi mwako. Alipokwisha kuyasema haya, pumzi ikamtoka.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akalalamika kwa sauti kubwa akisema: “Baba, ninatoa uzima wangu kwako.” Kisha kusema maneno haya, akakata roho.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho.