Luke 23:53 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaushusha kutoka msalabani, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limezikiwa mtu mwingine bado.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliushusha mwili kutoka msalabani na kuufunga kwenye nguo. Kisha akauweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika ukuta wa mwamba. Kaburi hili lilikuwa halijatumika bado.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha, akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia kitani safi na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo lilikuwa halijazikiwa mtu mwingine ye yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaushusha kutoka msalabani, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limezikiwa mtu mwingine bado.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akaushusha mwili huo kutoka msalabani, akauzungushia sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limetumika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaushusha msalabani, akaufunga kwa sanda, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajazikwa mtu bado ndani yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokwisha kuishusha toka juu ya musalaba, akaifungafunga na vitambaa na kuiweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika jiwe. (Ndani ya kaburi lile mulikuwa bado hamujazikwa mutu.)
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaushusha, akauzinga nguo za katani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani; hajawekwa mtu aliye yote ndani yake kamwe.