Luke 23:54 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilikuwa jioni Siku ya Maandalizi ya Sabato. Sabato ilikuwa ianze baada ya jua kuzama.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa siku ya maandalio, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na maandalio ya siku ya Sabato yalikuwa yanaanza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo siku ile ilikuwa ya andalio; ndipo, sikukuu ilipoanzia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ile ilikuwa ya matayarisho ya siku ya Sabato iliyokuwa karibu kuanza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ilikuwa siku ya Maandalio, sabato ikawadia.