Luke 24:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, “Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiwe peke yako mgeni huku Yerusalemu, ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa akasema, “Lazima wewe ni mtu pekee katika Yerusalemu ambaye hujui yaliyotokea huko.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, “Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, “Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwuliza, “Je, wewe ndiye peke yako mgeni huku Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiwe peke yako mgeni huku Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, “Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja wao, jina lake Kleofa, akajibu akimwambia: Wewe u mgeni peke yako Yerusalemu, usiyatambue yaliyokuwamo siku hizi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mumoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamujibu: “Kati ya wageni wanaokaa Yerusalema ni wewe tu usiyejua mambo yaliyotokea kule katika siku hizi?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemi, usiyajue yaliyokuwa ndani yake siku hizi?