Luke 24:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawajibu, “Mambo gani?” Wao wakamjibu, “Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo ya Isa Al-Nasiri. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Unasema kuhusu nini?” Wakasema, “Ni kuhusu Yesu, kutoka Nazareti, alikuwa nabii mkuu mbele za Mungu na watu wote. Alisema na kutenda mambo makuu mengi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akawajibu, “Mambo gani?” Wao wakamjibu, “Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawajibu, “Mambo gani?” Wao wakamjibu, “Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo ya Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo ya Isa Al-Nasiri. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawajibu, “Mambo gani?” Wao wakamjibu, “Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawauliza: Yapi? Ndipo, walipomwambia: Mambo ya Yesu wa Nasareti! Alikuwa mfumbuaji mwenye nguvu ya kutenda na ya kusema mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akawauliza: “Ni mambo gani?” Nao wakamujibu: “Haujui mambo yaliyomupata Yesu wa Nazareti? Yeye alishuhudiwa na Mungu na watu wote kwamba alikuwa nabii mwenye uwezo katika mambo aliyofanya na kusema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote;