Luke 24:36 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia “Amani iwe nanyi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa bado wanazungumza hayo, Isa mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wafuasi wawili wakiwa bado wanawaeleza mambo haya wafuasi wengine, Yesu mwenyewe akaja na kusimama katikati yao. Akawaambia, “Amani iwe kwenu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi wote wawili walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia “Amani kwenu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia “Amani iwe nanyi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati walipokuwa bado wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasimama katikati yao akasema, “Amani iwe nanyi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa bado wanazungumza hayo, Isa mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia “Amani iwe nanyi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokuwa wakiongea hivyo, mwenyewe akaja kusimama katikati yao, akawaambia: Tengemaneni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokuwa hawajamaliza kuwaelezea mambo hayo, mara moja Yesu mwenyewe akasimama katikati yao, na kuwaambia: “Amani kwenu!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Walipokuwa wakisema hivyo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akiwaambia, Amani kwenu.