Luke 24:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kungaa sana, wakasimama karibu nao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa wanashangaa kuhusu jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa kama umeme wakasimama karibu nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hawakulielewa hili. Walipokuwa wangali wanashangaa, watu wawili waliovaa mavazi yaliyong'aa walisimama pembeni mwao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kung'aa sana, wakasimama karibu nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kung'aa sana, wakasimama karibu nao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong'aa kama umeme wa radi, wakasimama karibu nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa kama umeme wakasimama karibu nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumetameta;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kungaa sana, wakasimama karibu nao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, walipopotelewa na jambo hili, mara wakawatokea watu wawili waliovaa nguo zimulikazo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipokuwa wakifazaika kwa ajili ya jambo hili, mara moja watu wawili waliovaa nguo zenye kungaa wakawatokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa wangali wakishangaa kwa haya, kumbe! watu wawili wakisimama karibu yao, wamevaa nguo za kumetameta.