Luke 24:47 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia Yerusalemu, yahubiriwe kwamba watu wanapaswa kutubu na kusamehewa dhambi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mliona mambo haya yakitokea, ninyi ni mashahidi. Na maandiko yanasema inawapasa mwende na kuwahubiri watu kuwa ni lazima wabadilike na kumgeukia Mungu, ili awasamehe. Ni lazima mwanzie Yerusalemu na mhubiri ujumbe huu kwa jina langu kwa watu wa mataifa yote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia na Yerusalemu yahubiriwe juu ya kutubu na kusamehewa dhambi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia Yerusalemu, yahubiriwe kwamba watu wanapaswa kutubu na kusamehewa dhambi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Toba na msamaha wa dhambi utatangazwa kupitia jina lake, kuanzia Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia Yerusalemu, yahubiriwe kwamba watu wanapaswa kutubu na kusamehewa dhambi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha wao wa mataifa yote watatangaziwa kwa Jina lake, wajute, wapate kuondolewa makosa; hivi vianzie Yerusalemu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Iliandikwa vilevile kwamba kwa jina lake watahubiri mataifa yote, kuanzia Yerusalema, kusudi wageuke toka katika zambi na wapate kusamehewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.