Luke 24:49 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tazama nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo kutoka juu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kumbukeni kwamba nitamtuma kwenu yule ambaye Baba yangu aliahidi. Kaeni jijini mpaka mtakapopewa nguvu hiyo kutoka mbinguni.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tazama nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapovikwa uwezo utokao juu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tazama, nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo utokao juu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hadi mvikwe uwezo utokao juu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtaniona mimi, nikituma kwenu kiagio cha Baba yangu! Lakini kaeni tu mjini, mpaka mtakapotiwa nguvu itokayo juu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mimi mwenyewe nitawatumia zawadi ile Baba yangu aliyoahidi ishuke juu yenu. Lakini mungojee kule Yerusalema mpaka mutakapojazwa uwezo kutoka juu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu.