Luke 3:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Yudea, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Uyahudi, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, ambapo: Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi; Herode alikuwa mtawala wa Galilaya; Filipo ndugu yake Herode alikuwa mtawala wa Iturea na Trakoniti; na Lisania, alikuwa mtawala wa Abilene.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti na Lisania akiwa mfalme wa Abilene,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwaka wa 15 wa kutawala kwake Kaisari Tiberio Pontio Pilato alikuwa mtawala nchi ya Yudea, naye Herode alikuwa mfalme wa Galilea, naye Filipo, ndugu yake, alikuwa mfalme wa Iturea na wa nchi ya Tarakoniti, naye Lisania alikuwa mfalme wa Abilene,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Uyahudi, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Tiberio mufalme wa Roma, Pontio Pilato alikuwa liwali wa jimbo la Yudea, na Herode alikuwa mutawala wa jimbo la Galilaya na ndugu yake Filipo alikuwa mutawala wa inchi ya Iturea na ya Tarakoniti. Vilevile Lisania alikuwa mutawala wa inchi ya Abilene,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,