Luke 3:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Askari wakamwuliza, “Vipi kuhusu sisi? Tufanye nini?” Akawaambia, “Msitumie nguvu au kutengeneza mashtaka ya uongo ili watu wawape pesa. Mtosheke na mishahara mnayopata.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Askari nao wakamwuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msimdhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtosheke na mishahara yenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao askari wakamwuliza, “Na sisi tufanye nini?” Naye akawajibu, “Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipomwuliza nao askari wakisema: Nasi tufanye nini? akawaambia: Msimwendee mtu kwa nguvu wala kwa ukorofi, tena mtoshewe na mishahara yenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo; tena mtoshewe na mshahara wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao waaskari wakamwuliza: “Na sisi, tufanye nini?” Naye akawajibu: “Musifanye ukorofi kwa mutu yeyote wala kumusingizia mutu, lakini mutoshelewe na mishahara yenu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Askari nao wakamwuliza wakisema, Nasi tufanyeni? Akawaambia, Msimtende jeuri mtu aliye yote, wala msitoze kitu bila haki; tena mwe radhi na mshsahara wenu.