Luke 3:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane, kuwa labda yeye ndiye Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yahya angeweza kuwa ndiye Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni mwao habari za Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mtu alitarajia kuja kwa Masihi, na walijiuliza wakisema, “Labda Yohana ndiye Masihi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane, kuwa labda yeye ndiye Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yahya angeweza kuwa ndiye Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza mioyoni mwao kuhusu Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wote walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu Yohane, kuwa labda yeye ndiye Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu walipokuwa wakingoja, vya Yohana vitakapotokea wazi, wote waliwaza mioyoni mwao kwamba: Yeye labda ni Kristo; ndipo, Yohana
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, watu walipokuwa wakingoja yatakayotokea, wote wakiwaza-waza mioyoni mwao habari za Yohana, kama labda yeye ndiye Kristo,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu walikuwa wakitazamia kuja kwa Kristo, na wote wakazania kwamba labda Yoane ndiye yeye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wale watu walipokuwa katika hali ya kutazamia, wakitafakari wote khabari za Yohana, kwamba yeye huenda akawa Kristo,