Luke 3:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye anacho mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka aipure nafaka yake, akusanye ngano katika ghala, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yuko tayari sasa kuja kusafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri na makapi, na kuiweka katika ghala yake kisha ataichoma ile isiyofaa katika moto usiozimika.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye ni kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka, aipure nafaka yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye anacho mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka aipure nafaka yake, akusanye ngano katika ghala, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye ungo wake uko mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanja wake wa kupuria, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye anacho mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka aipure nafaka yake, akusanye ngano katika ghala, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ungo wa kupepetea umo mkononi mwake, apafagie pake pa kupuria ngano; ngano atazikusanya, aziweke chanjani mwake, lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye pepeo lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake, na kuikusanya ngano ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anashika lungo katika mikono yake kwa kupepeta ngano. Atakusanya ngano na kuitia katika gala yake, lakini atateketeza maganda katika moto usiozimika.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; afakusanya nganu yake ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.