Luke 3:23 — Compare Translations

13 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipoanza kazi yake hadharani alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yusufu. Yusufu alikuwa mwana wa Eli,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipoanza kufundisha, alikuwa na umri kama wa miaka thelathini. Watu walidhani kuwa Yesu alikuwa Mwana wa Yusufu. Yusufu alikuwa mwana wa Eli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipoanza kazi yake hadharani, alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mwana wa Yosefu, mwana wa Heli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipoanza kazi yake hadharani alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Eli,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yusufu, Yusufu alikuwa mwana wa Eli,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri wa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipoanza kazi yake hadharani alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu walidhani yeye ni mtoto wa Yosefu mwana wa Heli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipoianza kazi yake alikuwa wa miaka kama 30. Akadhaniwa kuwa mwana wa Yosefu, wa Eli,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu, wa Eli,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae Yesu mwenyewe alipokuwa akianza kufundisha, umri wake amekuwa miaka thelathini, akidhaniwa kuwa mwana wa Yusuf, wa Eli,