Luke 3:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni barabara zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, yanyoosheni mapito yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ni kama maneno yaliyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya, yanayosema, “Kuna mtu anayeipaza sauti yake kutokea nyikani: ‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana; nyoosheni njia kwa ajili yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu imesikika jangwani: Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni barabara zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyosheni mapito yake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, yanyoosheni mapito yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndivyo ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni barabara zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, kama ilivyoandikwa kitabuni mwa maneno ya mfumbuaji Yesaya: Iko sauti ya mtu apigaye mbiu nyikani: Itengenezeni njia ya Bwana! Yanyosheni mapito yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya; Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi yakatimia maneno haya yaliyoandikwa katika kitabu cha maneno ya nabii Isaya: “Sauti inatangaza katika jangwa: ‘Mutengeneze njia ya Bwana, munyooshe pahali atakapopita!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kaina ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya, Sauti yake apigae mbiu jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake.