Luke 3:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyoshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitashushwa. Njia zilizopinda zitanyooshwa, na zilizoparuza zitasawazishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila bonde litajazwa, na kila mlima na kilima vitasawazishwa. Barabara zilizopinda zitanyooshwa, na barabara zenye mashimo zitasawazishwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyoshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima kitasawazishwa. Njia zilizopinda zitanyooshwa, zilizoparuza zitasawazishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitashushwa. Njia zilizopinda zitanyooshwa, na zilizoparuza zitasawazishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopindika patakuwa pamenyooka, Na palipoparuza patalainishwa;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyoshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vibonde vyote vifukiwe, navyo vilima vyote na vichuguu vyote vichimbuliwe! Napo palipopotoka panyoshwe, napo penye mashimo pawe njia za sawasawa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila bonde litajazwa, Na kila mlima na kilima kitashushwa; Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na palipoparuza patalainishwa;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivi kila bonde litafunikwa. Kila mulima na kila kilima vitasawanishwa. Njia zenye lukumba zitanyooshwa, nazo njia zenye mashimo zitalainishwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Killa bonde litajazwa, Na killa jabali na mlima utashushwra, Palipopotoka patakuwa pamenyoka, Na njia zilizoparuza zitakuwa njia sawa;