Luke 3:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kujisemea: ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka mawe haya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Badilisheni mioyo yenu! Kisha onesheni ya kuwa mmebadilika kwa namna mnavyoishi. Ninajua mtasema kuwa, ‘Ibrahimu ni baba yetu.’ Hilo halijalishi chochote. Ninawaambia Mungu anaweza kumwumbia Ibrahimu watoto kutokana na mawe haya!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema: Sisi ni watoto wa Abrahamu. Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyageuza mawe haya yawe watoto wa Abrahamu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kujisemea: ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaeni matunda yafananayo na toba yenu. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu. Kwa maana nawaambia, Mungu anaweza kumwinulia Abrahamu watoto kutoka katika mawe haya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi zaeni matunda yastahiliyo toba. Wala msianze kusema mioyoni mwenu kuwa, ‘Sisi tunaye Ibrahimu, baba yetu.’ Kwa maana nawaambia kuwa Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto kutoka mawe haya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Abrahamu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Abrahamu watoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kujisemea: ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tendeni mazao yaliyo ya kujuta kweli! Msianze kusema mioyoni mwenu: Tunaye baba yetu, ndiye Aburahamu! Kwani nawaambiani: Katika mawe haya ndimo, Mungu awezamo kumwinulia Aburahamu wana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi muonyeshe kwa njia ya matendo kwamba mumegeuka toka zambi zenu. Musianze tu kujisemesha kwamba Abrahamu ndiye babu yenu. Ninawaambia kwamba Mungu anaweza kugeuza mawe haya kuwa watoto wa Abrahamu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Zaeni, bassi, matunda yapatanayo na toba wala msianze kusema ndani ya nafsi zenu, Tunae baba ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambieni, ya kwamba Mungu katika mawe haya aweza kumwinulia Ibrahimu watoto.