Luke 4:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alitoka mtoni Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa, akiwa amejaa Roho Mtakatifu wa Mungu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho wa Mungu hadi nyikani,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akiwa amejaa Roho Mtakatifu, Yesu akarudi kutoka Mto Yordani. Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza mpaka nyikani
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alitoka katika mto Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alitoka mtoni Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa, akiwa amejaa Roho wa Mwenyezi Mungu, akarudi kutoka Yordani. Akaongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu hadi nyikani,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho kwa muda wa siku arobaini nyikani,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alitoka mtoni Yordani akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akaongozwa na Roho mpaka jangwani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akajaa Roho takatifu, akarudi akitoka huko Yordani, akapelekwa na Roho nyikani,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu, akarudia toka kwenye muto Yordani, akijazwa na Roho, na Roho huyo akamwongoza kwenda katika jangwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NA Yesu, akijaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani: akaongozwa na Roho kwenda jangwani, akijaribiwa na Shetani muda wa siku arubaini.