Luke 4:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Isa akarudi hadi Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho wa Mungu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alirudi Galilaya akiwa na nguvu za Roho Mtakatifu. Habari zake zilisambaa katika eneo lote lililozunguka Galilaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Isa akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho wa Mwenyezi Mungu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akarudi Galilea mwenye nguvu ya Roho, akavumika katika nchi zote zilizoko pembenipembeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akarudia Galilaya akijazwa na uwezo wa Roho, na habari zake zikaenea fasi zote katika pande zile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho hatta Galilaya, khabari zake zikaenea katika inchi yote iliyo kando kando.