Luke 4:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambia msemo huu: ‘Mganga jiponye mwenyewe,’ na pia mtasema: ‘Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye pia hapa kijijini mwako.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawaambia, “Ninafahamu mtaniambia mithali hii ya zamani: ‘Daktari, jitibu mwenyewe.’ Mnataka kusema ‘Tulisikia mambo yote uliyotenda Kapernaumu. Yatende pia hapa katika mji wako mwenyewe!’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambia msemo huu: Mganga jiponye mwenyewe, na pia mtasema: Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambia msemo huu: ‘Mganga jiponye mwenyewe,’ na pia mtasema: ‘Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye pia hapa kijijini mwako.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii, ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaambia, “Bila shaka mtatumia mithali hii: ‘Tabibu, jiponye mwenyewe! Mambo yale tuliyosikia kwamba uliyafanya huko Kapernaumu, yafanye na hapa kwenye mji wako.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Bila shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambia msemo huu: ‘Mganga jiponye mwenyewe,’ na pia mtasema: ‘Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye pia hapa kijijini mwako.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Kweli mtaniambia fumbo hili: Mganga, jiponye mwenyewe! Hata huku kwako, ulikokulia, yafanye, tuliyoyasikia, ya kuwa yamefanyika Kapernaumu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaambia: “Hakika mutaniambia fumbo hili: ‘Muganga, ujiponyeshe wewe mwenyewe!’ Na vilevile mutaniambia hivi: ‘Tumesikia mambo yote uliyotenda katika muji Kapernaumu, basi uyafanye hapa vilevile katika muji wako.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia methali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako: mambo yote tuliyosikia yametendeka Kapernaum, yatende na hapa pia katika inchi yako mwenyewe.