Luke 4:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yesu akasema, “Ukweli ni huu, nabii hakubaliki katika mji wa kwao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika kwenye mji wake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akasema, “Amin, nawaambia, hakuna nabii anayekubalika katika mji wake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii anayekubaliwa katika nchi yake mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akasema: Kweli nawaambiani: Hakuna mfumbuaji anayepokelewa kwao, alikokulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akaongeza kusema: “Kweli ninawaambia: hakuna nabii anayekubaliwa katika muji wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Amin, nawaambieni, Hapana nabii apatae kukubaliwa katika inchi yake mwenyewe.