Luke 4:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Ilya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wa Eliya mvua haikunyesha katika Israeli kwa miaka mitatu na nusu. Chakula hakikuwepo mahali popote katika nchi yote. Palikuwa wajane wengi katika Israeli wakati huo. Lakini Eliya hakutumwa kwenda kwa mmoja wa wajane waliokuwa katika Israeli bali kwa mjane aliyekuwa katika mji wa Sarepta, jirani na Sidoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Eliya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Ilya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia katika nchi nzima;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawaambiani ya kweli: Siku za Elia kulikuwa na wajane wengi katika Waisiraeli; ni hapo, mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, ikawa njaa kubwa katika nchi zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninawaambia ukweli: kulikuwa wajane wengi katika inchi ya Israeli katika siku za nabii Elia. Wakati ule, mvua ilifungwa isinyeshe kwa muda wa miaka mitatu na nusu na kukakuwa njaa kubwa katika inchi yote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini kwa kweli nawaambieni, Palikuwa wajane wengi katika Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita; njaa kuu ikaingia inchi yote: