Luke 4:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima ambao mji huo ulikuwa umejengwa juu yake, ili wamtupe chini kutoka mteremko mkali.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakasimama na kumlazimisha Yesu atoke nje ya mji. Mji wao ulijengwa juu ya kilima. Wakamchukua Yesu mpaka ukingo wa kilima ili wamtupe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mtelemko mkali.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hadi kwenye kilele cha mlima mahali ambapo mji huo ulikuwa umejengwa, ili wamtupe chini kutoka kwenye mteremko mkali.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakainuka, wakamfukuza mjini, wakampeleka ukingoni pa mlima, ambao mji wao ulikuwa umejengwa juu yake, wapate kumsukuma chini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakasimama, wakamusukuma Yesu hata inje ya muji wao, uliojengwa juu ya kilima. Wakamupeleka kwenye maporomoko kusudi wamutupe chini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakamchukua hatta ukingo wa kilima kile kilichojengwa mji wao, wapate kumporomosha: