Luke 4:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akaja akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Yule mama akainuka mara, akawatumikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Isa akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka mara moja, naye akaanza kuwahudumia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alisimama karibu yake na kuiamuru homa kuondoka. Homa ikamwacha, naye akasimama na kuanza kuwahudumia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akaenda akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Mara yule mama akainuka, akawatumikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akaja akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Yule mama akainuka mara, akawatumikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Yesu akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka saa ile ile akaanza kuwahudumia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Isa akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka saa ile ile, naye akaanza kuwahudumia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akainuka, akawatumikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akaja akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, nayo ikamwacha. Yule mama akainuka mara, akawatumikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaja, akasimama kichwani pake, akaikaripia homa; ndipo, ilipomwacha. Papo hapo akainuka kitandani, akawatumikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasimama karibu naye, akaikemea ile homa, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi akainama kunapokuwa yule mama, akaamuru ile homa itoke ndani yake, naye akapona. Na mara moja akasimama na kuanza kuwashugulikia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasimama karibu nae akaikemea ile homa, ikamwacha; marra akaondoka akawakhudumu.