Luke 4:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake asubuhi, Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta. Hao watu walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake, kulipopambazuka, Isa alienda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafuta-tafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata Yesu alijitenga na kwenda mahali ili awe peke yake. Watu wakawa wakimtafuta. Walipompata, walijaribu kumzuia asiondoke.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesho yake asubuhi Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta, na walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake asubuhi, Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta. Hao watu walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake, kulipopambazuka, Isa alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, nao walipomwona wakajaribu kumzuia asiondoke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafutatafuta, na walipomfikia, wakataka kumzuia asiondoke kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake asubuhi, Yesu aliondoka akaenda mahali pa faragha. Watu wakawa wanamtafuta. Hao watu walipofika mahali alipokuwa, wakajaribu kumzuia ili asiondoke kwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kulipokucha, akatoka, akaenda mahali palipokuwa pasipo watu. Ndipo, makundi ya watu walipomtafuta, wakaja kwake, wakamzuia, asiondoke kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafuta-tafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokucha kesho yake, Yesu akatoka katika muji na kwenda pahali penye ukiwa. Kundi kubwa la watu wakaanza kumutafuta. Nao walipomwona walitaka kumuzuia kusudi asitoke kwao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta ulipokuwa mchana akatoka akaenda mahali pasipokuwa na watu: makutano wakamtafutatafuta, wakamfikilia, wakataka kumzuia asiondoke kwao.