Luke 4:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonesha milki zote za dunia kwa mara moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha mwovu akamchukua Yesu na kwa muda mfupi akamwonyesha falme zote za ulimwengu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonyesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ibilisi akampeleka hadi juu ya mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia kwa mara moja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akampandisha juu, akamwonesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akampandisha mlimani, akamwonyesha kwa kitambo kidogo ufalme wote pia wa ulimwengu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Shetani akamupeleka kwenye nafasi inayoinuka juu sana. Akamwonyesha mara moja falme zote za dunia,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Shetani akampandisha juu ya mlima mrefu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.