Luke 4:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwovu akamwambia, “Nitakufanya uwe mfalme wa sehemu zote hizi. Utakuwa na mamlaka juu yao, na utapata utukufu wote. Yote yametolewa kwangu. Ninaweza kumpa yeyote kadri ninavyopenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa ye yote ninayetaka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwambia, “Nitakupa mamlaka juu ya milki hizi na fahari zake zote, kwa maana zimekabidhiwa mkononi mwangu nami ninaweza kumpa yeyote ninayetaka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Msengenyaji akamwambia: Nguvu hii yote na utukufu wake nitakupa wewe; kwani mimi nimepewa, nami humpa ye yote, nimtakaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kumwambia: “Nitakupa falme hizo zote zenye uwezo na utukufu, kwa maana mimi nimezipewa zote, nami ninaweza kuzitoa kwa mutu yeyote ninayetaka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Shetani akamwambia, Nitakupa mamlaka haya yote, na fakhari yake: kwa kuwa nimekabidhiwa, nami nampa ye yote nimtakae: