Luke 4:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, na kumtumikia yeye peke yake.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Ni lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamjibu, “Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako, na utamtumikia yeye peke yake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, na kumtumikia yeye peke yake.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mwabudu Bwana Mwenyezi Mungu wako na umtumikie yeye peke yake.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako, na kumtumikia yeye peke yake.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akajibu akimwambia: Ondoka nyuma yangu, Satani! Imeandikwa: Umwangukie Bwana Mungu wako na kumtumikia peke yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yesu akamujibu: “Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umutumikie yeye peke yake.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamwambia, Nenda zako nyuma yangu, Shetani: maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.