Luke 5:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu yeyote, bali nenda ukajioneshe kwa kuhani na ukatoe sadaka alizoagiza Musa kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamkataza asimwambie mtu, ila, Nenda ukajionyeshe kwa kuhani; ukatoe kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamwambia, “Usimwambie mtu yeyote kilichotokea. Lakini nenda kwa kuhani akakuchunguze. Na umtolee Mungu sadaka ambazo Musa aliamuru watu wanaoponywa watoe, ili iwe ushahidi kwa watu kwamba umepona.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama inavyotakiwa na Sheria ya Mose, iwe uthibitisho kwao kwamba umepona.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu ye yote, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani na ukatoe dhabihu alizoagiza Mose ili kuwa ushuhuda kwao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamwagiza akisema, “Usimwambie mtu yeyote, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani na ukatoe sadaka alizoagiza Musa kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamkataza asimwambie mtu, ila, Nenda ukajioneshe kwa kuhani; ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamkataza, asimwambie mtu neno, akasema: Uende zako, ujionyeshe kwa mtambikaji, utoe kipaji kwa ajili ya kutakaswa kwako, kama Mose alivyoagiza, kije kinishuhudie kwao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamkataza asimwambie mtu, ila, Nenda ukajionyeshe kwa kuhani; ukatoe kwa ajili ya kutakasika kwako kama Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamwamuru hivi: “Usimwambie mutu neno juu ya hii. Lakini kwenda na kumwonyesha kuhani jinsi unavyokuwa sasa. Kisha utoe sadaka kama Musa alivyoamuru, kuwa ushuhuda kwa watu wote kwamba umetakaswa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwagiza asimwambie mtu: illa enenda, ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe kwa kutakasika kwako alivyoamuru Musa, illi kuwa ushuhuda kwao.