Luke 5:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini habari zake Isa zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makundi makubwa ya watu walikuwa wakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini habari kuhusu Yesu zilizidi kuenea zaidi. Watu wengi walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini habari zake Yesu zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wo wote, makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini habari zake Isa zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini uvumi wake ukafuliza kuendelea, wakakusanyika makundi ya watu wengi, wamsikilize wakiponywa magonjwa yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivi habari juu ya Yesu zikazidi kuvuma na makundi mengi ya watu wakakusanyika kwa kumusikiliza na kuponyeshwa magonjwa yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.