Luke 5:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara watu wakaja, wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani, wamweke mbele ya Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwepo mtu aliyepooza na baadhi ya watu walikuwa wamembeba kwenye machela. Walijaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara watu wakaja wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani wamweke mbele ya Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara watu wakaja, wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani, wamweke mbele ya Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara watu wakaja, wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani, wamweke mbele ya Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo wakaja watu wakileta mtu aliyelala kitandani mwenye ugonjwa wa kupooza. Wakajaribu kumwingiza nyumbani na kumweka mbele yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, wakaja watu wanamchukua kitandani mtu mwenye kupooza; wakataka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja wakakuja wakimubeba mutu aliyepooza juu ya kipoyi. Wakatafuta njia ya kumwingiza ndani ya nyumba kusudi wamuweke mbele ya Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kumbe! watu wanachukua mtu kitandani mwenye kupooza: wakitaka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.