Luke 5:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya paa, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya matofali, wakamteremsha yule mgonjwa kwa mkeka wake hadi katikati ya umati ule pale mbele ya Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini walishindwa kufika alipokuwa Yesu kwa sababu kulikuwa na watu wengi sana. Hivyo walikwenda juu ya paa ya nyumba na kumshusha aliyepooza chini kupitia tundu kwenye dari. Waliishusha machela alimokuwa aliyepooza kwa usawa kiasi kwamba akawa amelala mbele ya Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya dari, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya paa, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya vigae, wakapata nafasi ya kumtelemsha yule mgonjwa kwa mkeka wake katikati ya ule umati pale pale mbele ya Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya matofali, wakamteremsha yule mgonjwa kwa mkeka wake hadi katikati ya ule umati pale mbele ya Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampitisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini, kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya paa, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wasipoona pa kumwingizia kwa ajili ya watu wengi wakapanda katika paa la nyumba, wakafumua vigae, wakamshusha hapo pamoja na kitanda chake, wakamweka katikati mbele ya Yesu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata walipokosa nafasi ya kumpeleka ndani kwa ajili ya lile kundi la watu, walipanda juu ya dari wakampisha katika matofali ya juu, wakamshusha yeye na kitanda chake katikati mbele ya Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa kuona walikosa njia ya kumwingiza ndani, kwa sababu ya wingi wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondosha matebura na kumushusha yule mugonjwa katikati ya watu, akiwa juu ya kipoyi chake, hata wakamufikisha mbele ya Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta walipokosa pa kumpeleka ndani kwa sababu ya lile kundi la watu, wakapanda juu ya dari wakampisha katika matofali, wakamshusha na kitanda chake hatta katikati mbele ya Yesu.