Luke 5:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waalimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu anayesema maneno ya kufuru? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mafarisayo na wale walimu wa Torati wakaanza kuuliza, “Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? N'nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wao kwa wao wakisema: “Huyu mtu ni nani kiasi cha kuthubutu kusema hivi? Si anamtukana Mungu! Mungu peke yake ndiye anayesamehe dhambi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walimu wa Sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu anayemkufuru Mungu kwa maneno yake? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waalimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu anayesema maneno ya kufuru? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mafarisayo na wale walimu wa sheria wakaanza kuuliza, “Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya makufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mafarisayo na wale walimu wa Torati wakaanza kuuliza, “Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wale Waandishi na Mafarisayo wakaanza kuulizana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waalimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu anayesema maneno ya kufuru? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, waandishi na Mafariseo walipoanza kuwaza wakisema: Nani huyu anayesema maneno ya kumbeza Mungu? Yuko nani awezaye kuondoa makosa? Siye Mungu peke yake tu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kuhojiana wakisema, Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? N’nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walimu wa Sheria na Wafarisayo wakaanza kujiuliza: “Ni mutu gani huyu anayemutukana Mungu? Ni nani anayeweza kusamehe zambi, isipokuwa Mungu peke yake?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu?