Luke 5:24 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kusamehe dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako uende zako nyumbani.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ili mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi,” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, Simama, chukua mkeka wako uende nyumbani kwako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kusudi mpate kujua, ya kuwa Mwana wa mtu ana nguvu ya kuondoa makosa nchini, akamwambia mwenye kupooza: Nakuambia: Inuka, jitwishe kitanda chako, uende nyumbani kwako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ninataka mujue kwamba Mwana wa Mutu yuko na mamlaka ya kusamehe zambi hapa katika dunia.” Kwa hiyo akamwambia yule mutu aliyepooza: “Ninakuamuru, simama, utwae kipoyi chako na urudie kwako.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dhambi (alimwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako.