Luke 5:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda nyumbani kwake huku akimtukuza Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake, akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara hiyo akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yule mtu akasimama saa ile ile mbele ya kila mtu. Akaubeba machela yake na kwenda nyumbani kwake, akimsifu Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda zake nyumbani huku akimtukuza Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda nyumbani kwake huku akimtukuza Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake, akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara hiyo akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda nyumbani kwake huku akimtukuza Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo akainuka machoni pao, akajitwisha kitanda, alichokilalia, akaenda nyumbani kwake akimtukuza Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara hiyo akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, huku akimtukuza Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pale pale mutu yule akasimama mbele yao wote, akatwaa kipoyi alichokilalia, akaenda kwake akimusifu Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra akasimama mbele yao, akajitwika kile alichokilalia, akaenda zake nyumbani kwake, akimhimidi Mungu.