Luke 5:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliingia kwenye mashua ya Simoni. Akamwomba Simoni aisogeze mbali kidogo na ufukwe wa ziwa. Kisha akaketi ndani ya mashua na akawafundisha watu waliokuwa ufukweni mwa ziwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja, iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka pwani. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaingia katika mashua moja, ndiyo yake Simoni, akamtaka aipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano akiwa katika mashua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipoingia katika chombo kimoja kilichokuwa cha Simoni, akamwomba, akisogeze mbali kidogo hapo ufukoni. Akakaa katika chombo akiwafundisha makundi ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaingia katika chombo kimoja, ndicho chake Simoni, akamtaka akipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano ali chomboni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akaingia ndani ya moja kati ya vile vyombo, nacho kilikuwa cha Simoni. Yesu akamwomba akisukume mbali kidogo na kivuko. Halafu akaikaa mule na kuwafundisha watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaingia chombo kimoja, kilichokuwa cha Simon, akamtaka asogeze kidogo kutoka pwani. Akakaa, akawafundisha makutano katika chombo.