Luke 5:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengine wakamwambia, “Wafuasi wa Yohane Mbatizaji hufunga mara kwa mara na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwambia Isa, “Wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wakamwambia, Wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadhi ya watu wakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohana hufunga na kuomba mara kwa mara, vivyo hivyo wafuasi wa Mafarisayo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa kila wakati.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wengine wakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohane mbatizaji hufunga mara nyingi na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengine wakamwambia, “Wafuasi wa Yohane Mbatizaji hufunga mara kwa mara na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwambia Yesu, “Wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwambia Isa, “Wanafunzi wa Yahya na wa Mafarisayo mara kwa mara hufunga na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wakamwambia, Wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengine wakamwambia, “Wafuasi wa Yohane Mbatizaji hufunga mara kwa mara na kusali; hata wafuasi wa Mafarisayo hufanya vivyo hivyo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wakamwambia: Wanafunzi wa Yohana hukaza kufunga na kuomba, vilevile nao wanafunzi wa Mafariseo, lakini wanafunzi wako hula, hunywa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wakamwambia, Wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja wakamwambia Yesu: “Wanafunzi wa Yoane na wale wa Wafarisayo wanafunga mara nyingi na kuomba, lakini wanafunzi wako wanaendelea kula na kunywa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao wakamwambia, Kwa nini wanafunzi wa Yohana wanafunga marra nyingi na kusali, na wanafunzi wa Mafarisayo wanafanya vilevile, bali wanafunzi wako hula na hunywa?