Luke 5:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna mtu anayetamani kunywa divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani kwani husema ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, bali husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna mtu ambaye baada ya kunywa divai ya zamani hutaka divai mpya. Kwa sababu husema, ‘Divai ya zamani ni nzuri.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wala hakuna mtu ambaye hutamani kunywa divai mpya baada ya kunywa ya zamani, kwani husema: Ile ya zamani ni nzuri zaidi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna mtu anayetamani kunywa divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani kwani husema ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wala hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani, bali husema, ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna mtu anayetamani kunywa divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani kwani husema ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala hakuna aliyekunywa mvinyo ya kale, akitaka mpya, kwani husema: ile ya kale ndiyo nzuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hakuna anywaye divai ya kale akatamani divai mpya; kwa kuwa asema, Ile ya kale ndiyo iliyo njema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna mutu aliyekwisha kunywa divai ya zamani atakayetaka tena divai mupya. Kwa maana anasema kwamba ile ya zamani ni nzuri zaidi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wala hakuna mtu anywae divai ya kale, marra akatamani divai mpya, maana asema, Ile ya kale ni njema zaidi.