Luke 6:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikawa siku moja ya Sabato Isa alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, nao wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati fulani siku ya Sabato, Yesu alikuwa akitembea kupitia katika baadhi ya mashamba ya nafaka. Wafuasi wake wakachukua masuke, wakayapukusa mikononi mwao na kula nafaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa siku moja ya Sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikawa siku moja ya Sabato Isa alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, nao wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusapukusa mikononi mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano, na wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano, wakaondoa punje zake kwa mikono, wakala.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawa akipita katika mashamba siku ya mapumziko; l nao wanafunzi wake wakakonyoa masuke, wakayafikicha kwa mikono, wakala.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusa-pukusa mikononi mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja ya Sabato, Yesu akapita katika mashamba ya ngano, wanafunzi wake wakaanza kuchumachuma masuke ya ngano, wakayasiritasirita katika mikono yao na kuyakula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
IKAWA siku ya Sabato alikuwa akipita katika makonde, wanafunzi wake wakavunja masuke, wakayala, wakiyapukusapukusa mikononi mwao.