Luke 6:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Asubuhi iliyofuata aliwaita wafuasi wake, akachagua kumi na wawili miongoni mwao na kuwaita Mitume. Nao ni:
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akachagua kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulipopambazuka akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kulipokucha aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita mitume;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulipokucha, akawaita wanafunzi wake, akachagua miongoni mwao kumi na wawili; ndio aliowapa jina la Mitume.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kulipokuwa mchana aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita Mitume;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulipokucha, akawaita wanafunzi wake, na kuchagua hawa kumi na wawili katikati yao, akawapanga jina la mitume:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ulipokuwa mchana akawaita wanafunzi wake: akachagua watu thenashara miongoni mwao, ambao aliwaita mitume.