Luke 6:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Yudea, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Uyahudi wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu na mitume wakatelemka kutoka mlimani. Yesu akasimama mahali tambarare. Kundi kubwa la wafuasi wake lilikuwa pale. Walikuwepo pia watu wengi waliotoka sehemu zote za Uyahudi, Yerusalemu, na maeneo ya pwani karibu na Tiro na Sidoni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kushuka mlimani pamoja na mitume, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo palikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akashuka pamoja nao akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, Yerusalemu na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Yudea wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanda; hapo palikuwa na kundi zima la wanafunzi wake wengi na watu wengine wengi sana waliotoka Yudea po pote na Yerusalemu na pwani pa Tiro na Sidoni;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Uyahudi wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akashuka toka kilima pamoja na wanafunzi wake, na kusimama kwenye uwanja. Pale kulikuwa wanafunzi wake pamoja na kundi kubwa sana la watu waliotoka Yerusalema, katika Yudea yote na pande za miji Tiro na Sidona pembeni ya bahari.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao;