Luke 6:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu watawachukia kwa sababu ninyi ni wa milki ya Mwana wa Adamu. Watawabagua na watawatukana. Watajisikia vibaya hata kutamka majina yenu. Mambo haya yatakapotukia, mjue kuwa baraka kuu ni zenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Heri yenu ninyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wenye shangwe ni ninyi, watu watakapowachukia na kuwatenga kwao na kuwatukana na kuyakataa majina yenu kwa kuwa mabaya kwa ajili ya Mwana wa mtu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Heri ninyi wakati watu wanapowachukia, wanapojitenga nanyi, wanapowatukana na kuchafua jina lenu kwa ajili ya Mwana wa Mutu!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu.